9 Agosti 2026 - 12:18
Msemaji wa IRGC: Tutaendelea kushikilia Mlango wa Hormuz hadi adui akubali masharti yetu yote

Brigedia Jenerali Mohbi amesema Iran itaendelea na mapambano hadi kufikia ushindi wa mwisho, akisisitiza kuwa waandishi wa habari walikuwa na nafasi muhimu katika kujenga uelewa wa ushindi, kuimarisha utamaduni wa upinzani na kudumisha umoja wa wananchi.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), Brigedia Jenerali Mohibi, amesema kuwa Iran itaendelea kushikilia Mlango wa Hormuz** hadi adui akubali masharti yote ya Iran.
 
Brigedia Jenerali Mohbi amesema kuwa vita pekee ambavyo Marekani ilikiri wazi kushindwa na kutopata mafanikio yoyote ni “Vita vya Ramadhani”, akisisitiza kuwa jambo hilo limeifanya Iran kuendelea na mapambano hadi kufikia ushindi wa mwisho.
 
Amesema uzoefu huo umeimarisha azma ya Iran ya kuendelea na njia ya upinzani na kutorudi nyuma hadi malengo yake yatimie.
 
Waandishi wa habari na nafasi yao katika vita
 
Brigedia Jenerali Mohibi pia amewapongeza waandishi wa habari kwa utendaji wao wakati wa vita vya siku 12 na Vita vya Ramadhani, akisema walitimiza jukumu muhimu katika medani hizo.
 
Ameeleza kuwa miongoni mwa mambo muhimu zaidi yaliyotekelezwa na waandishi wa habari ni kujenga uelewa wa umma kuhusu ushindi na umuhimu wa upinzani, jambo alilolitaja kuwa sehemu muhimu ya utendaji wao katika kipindi hicho.
 
Aidha, amesema waandishi walifanikiwa kufuatilia na kuwasilisha ujumbe wa kuendeleza na kueneza utamaduni wa upinzani na kukabiliana na maadui, pamoja na kuwahamasisha wananchi kubaki katika uwanja wa mapambano.
 
Kwa mujibu wa msemaji huyo, umoja na mshikamano wa wananchi pia ulikuwa miongoni mwa ujumbe muhimu ambao waandishi wa habari waliufuatilia na kuutekeleza kwa mafanikio katika kipindi hicho.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha